Tukio hilo linadaiwa kutokea juzi, ambapo Dk huyo anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 50 (jina limehifadhiwa), alikamatwa saa 10:45 alasiri katika nyumba ya mjomba wake iliyopo eneo la Kiboriloni mjini hapa akiwa katika harakati za kufanya tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz aliwaambia wanahabari jana kuwa, uchunguzi umebaini msichana aliyekuwa akitolewa mimba ni mhitimu wa Chuo cha Ualimu Masama Suni.
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, msichana huyo amelazwa katika Hospitali ya Mawenzi akiendelea kupatiwa matibabu baada ya jaribio hilo la kumtoa mimba kuzimwa na polisi kabla halijakamilika.

No comments:
Post a Comment